Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka wachezaji wanaoliwakilisha taifa katika mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Uingereza na michezo ya Afrika nchini Misri kwenda kulipambania taifa kwa kurudi na ushindi katika mashindano hayo wakati wa kuziaga na kuzikabidhi bendera ya taifa timu hizo leo julai 20, 2022 . Waziri mwenye dhamana  amedokeza na kusema  Serikali imetenga dola elfu 22,000 kwa wanamichezo watakaotwaa medali ya fedha, dhahabu, na shaba kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola inayotarajiwa kuanza tarehe 28 Julai hadi 08 Agosti, 2022 nchini Uingereza, kila atakayeleta medali ya dhahabu atapewa bonasi ya dola 10,000, medali ya fedha dola 7000 na medali ya shaba dola 5000.