Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Henry Tandau akikabidhi Bendera ya Taifa kwa nahodha wa timu ya Tanzania kwa michezo ya pili ya Afrika ya Ufukweni Jaruph Rajabu katika sherehe fupi iliyofanyika katika hoteli ya Chichi Kinondoni tarehe 23 June 2023 kuiga timu hiyo. Michezo ya pili ya Afrika ya Ufukweni itafanyika katika mji wa Hammamet, nchini Tunisia kuanzia 24 hadi 30 Juni 2023.