Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Baraza la michezo la Taifa (BMT), Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kwa kushirikiana na United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO) imeandaa semina ya elimu kuhusu matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni kwa vyama vya michezo, walimu wa shule na maafisa michezo wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam.