Leo, Tarehe 4/12/2024 Kamisheni ya uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania imetangaza rasmi tarehe ya uchaguzi na kutoa muongozo wa uchaguzi wa viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania kwa mwaka 2025-2028. Uchaguzi utafanyika rasmi, Jumamosi ya tarehe 14/12/2024 Katika ukumbi uliopo DODOMA HOTEL. Aidha Kamisheni ya uchaguzi imesema kuwa nafasi zitakazoshindaniwa ni 12 ambazo ni ;Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania na nafasi 10 za Ujumbe wa Kamati za utendaji. Katika nafasi za wajumbe nafasi 5 za Tanzania bara na 5 za Zanzibar. Katika nafasi 5 za ujumbe kwa Tanzania bara na Zanzibar nafasi 2 ni lazima ziwe za wanawake. Baada ya maelezo hayo Kamisheni ya uchaguzi imesema kuwa fomu za uchaguzi zipo tayari na zitaanza kutolewa hapo kesho tarehe 5/11/2024-11/11/2024 kwa Tanzania bara fomu zinapatikana ofisi za Kamati ya Olimpiki Tanzania zilizopo Mwananyamala, Komakoma na kwa Zanzibar fomu zinapatikana katika ofisi za, Diabetics Association Zanzibar zilizopo mtaa wa Mpendae kwa binti Amrani. Hivyo Kamisheni ya uchaguzi imesisitiza wananchi kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali zilizotangazwa.