VIONGOZI wa michezo nchini wametakiwa kuwa na kanuni za wazi za fedha katika vyama au mashirikisho yao ili kuweka uwazi kwa wadau mapato na matumizi ya fedha.

Hayo yameelezwa na Mwanasheria Msomi, Ibrahim Mkwawa katika warsha ya Utawala bora kwa Viongozi wa Mashirikisho na Vyama vya Michezo nchini.

Anasema kuwa mashirikisho ya Michezo ya kimataifa yanataka vyama vyetu vya kitaifa lazima kuwa na watia saini zaidi ya mmoja ili kupunguza matatizo mabaya ya fedha.

Naye Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau amesema kuwa Mashirikisho ya Michezo pia yanatakiwa kuwa na mipango au utaratibu wa vita dhidi ya dawa zinazopigwa marufuku michezoni (doping).

Anasema suala hilo kwa sasa limekuwa linapigwa vita dunia nzima kutokana na hathari zake, ikiwemo kuharibu afya ya wachezaji wanaotumia dawa hizo na kwa wanawake wamekuwa hata wakipoteza maoumbo au maumbile yao ya asili na kuwa kama wanaume.