Mkimbiaji wa marathon kwa wanawake J a c k l i n e S a k i l u afanya kilichofanyika na mwanariadha Mtanzania mwingine John Stephen Akhwari katika mashindano ya marathon katika Michezo ya Olimpiki mwaka 1968 huko Mexico City.
Sakilu, akiwa na Mtanzania Mwenzake Failuna Matanga (huyu alimaliza wa tano) alishindana katika mbio za marathon kwa wanawake za Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Birmingham, Uingereza.
Akiwa bega kwa bega na washindani wenzake katika mbio hizo ngumu za kilomita 42, Sakilu akapatwa na maumivi makali ya msuli wa nyuma ya paja lake la kushoto wakati wakiwa wamekimbia kilomita 14. Walipofika kilomita 17 maumivu yakazidi ukali ikabidi asimame kwa muda kisha akaendelea kwa kuchechemea, akiachwa nyuma na wenzake.
Lakini shujaa huyu mwenye umri wa miaka 36 hakukata tamaa na wala hakujitoa mashindanoni. Akafanya kama John Stephen Akhwari alivyofanya miaka 54 iliyopita, kuendelea na mashindano toka msuli ulipomshika akiwa kilomita 19 tu za mbio hizo na kumaliza wa mwisho. Alipoulizwa kwa nini hakujitoa Akhwari akawajibu: “Nchi yangu ilinituma maili 5,000 zote hizi ili kuanza mbio, ilinituma maili 5,000 hizi nimalize mbio…”
Ushujaa huo wa Akhwari unatambulika na kuheshimiwa ulimwenguni kote, na umekuwa gumzo na kutolewa mfano mara kwa mara kimataifa.
Sakilu naye akaendelea na mashindano kwa kuchechemea huku akiugulia maumivu makali kwa kilomita 25 zote zilizosalia, akipigania heshima ya nchi yake iliyomtuma kushindana.
Sakilu alimaliza mbio hizo akiwa wa mwisho lakini alishangiliwa sana na umati wa watu kama vile ni mshindi. Clip hio inajieleza.
Recent Comments