Mwanariadha wa Kimataifa Alphonce Felix Simbu Amenyakua Medali ya Fedha ,kwa kukimbia muda wa Saa Mbili na dakika kumi na mbili na Sekunde ishirini na Tisa (2:12:29) , kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola , yaliyofanyika Jijini Birmingham nchini Uingereza Tarehe 30 Julai 2022.
Medali aliyoshinda Shimbu ni ya kwanza tokea mwaka 2006, wakati mkimbiaji Samson Ramadhani aliposhinda medali ya dhahabu michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Melbourne, Australia.
Mwaka huo huo wa 2006 mkimbiaji Fabian Joseph pia alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 10,000 huko huko Australia.
Recent Comments