Timu ya Tanzania iliyoshiriki michezo ya 22 ya jumuiya ya madola na kufanikiwa kuleta medali tatu nyumbani yakaribishwa rasmi na waziri mwenye dhamana ya michezo Tanzania Mohamed Mchengerwa na kuwakabidhi vyeti wachezaji mashujaa walioshika nafasi kuanzia namba moja hadi nane kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola iliyomalizika hivi karibuni jijini Birmingham Uingereza.

Kiongozi wa wachezaji Alphonce Felix Simbu amemshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kwa utayari wa kuwekeza katika Michezo. Aidha, ameishukuru Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kusimamia vizuri Michezo na kuomba kuwa huo uwe mwanzo wa kuendelea kujiandaa ili kufuzu kwenye mashindano makubwa.
Ameyaomba majeshi kufufua Michezo kama ilivyokuwa awali ili kuwa na wachezaji wengi zaidi.