Rais Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Gullam Abdullah Rashid (walioketi wa pili kulia) na Katibu Mkuu wake Bw. Filbert Bayi walipowatembelea kuwajulia hali na kuwatia moyo wachezaji kambini kwao katika kijiji cha wanamichezo kilicho katika Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, ambako mashindano ya jumuiya ya madola  yatafunguliwa rasmi mjini Birmingham siku ya Alhamisi Julai 28, 2022. Wengine walioketi nao ni Makamu wa Rais wa TOC Bw. Henry Tandau ambaye ndiyo kiongozi wa msafara (wa pili kushoto) na Meneja wa timu Suleiman Jabir Mahmoud (kushoto).