Kassim Selemani Mbundwike aka Mfupa wa Sokwe ameshinda kwa RSC ama Refa Kusimamisha pambano katika
round ya tatu ya pambano lake la Robo fainali dhidi ya Marion Faustino AH Tong kutoka nchi ya Samoa katika bout no. 162 katika uzani wa Light middleweight 67kg – 71kg
Na tayari Mfupa huo wa Sokwe umejihakikishia kupata medali ambayo itakua ya pili kwa upande wa Ngumi, na ya tatu kwa Team Tanzania katika Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Birmingham, Uingereza.
Mbundwike anajiunga na askari mwenzie wa JWTZ mwenye cheo kama yeye cha ‘Private’, Yusufu Changalawe, katika mpambano wa nusu fainali siku ya Jumamosi na kama wakishinda wataingia fainali Jumapili kugombea
Medali za dhahabu ama Fedha.