Kamati ya Olimpiki Tanzania imeadhimisha siku ya Olimpiki Kitaifa tarehe 8/7/2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Michezo wa rika zote wadogo kwa wakubwa. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa Mwaka huu ikisema “Let’s Move,” kauli ambayo inadhamiria kuhamasisha jamii kufanya mazoezi kwa ajili ya kutunza afya zao na kuweka miili yao sawa. Adhimisho hilo la siku ya Olimpiki Kitaifa limehusisha michezo mbalimbali ikiwemo mbio za taratibu za kilomita 2.5 kwa Watoto chini ya miaka 14 na kilomita 5.0 kwa walio na miaka 15 na kuendelea, Aerobics, Breaking,Teqball pamoja na mchezo wa Skateboard.