Kamati ya Olimpiki Tanzania itaadhimisha Siku ya Olimpiki kitaifa hapo tarehe 08/07/2023, kuanzia saa 12.00 asubuhi mpaka saa 7.00 mchana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Lets Move” kauli ambayo inadhamiria kumhamasisha kila mtu kufanya mazoezi kwa ajili ya afya na kuuweka mwili sawa.

Sherehe hiyo itahusisha mbio za taratibu za kilomita 2.5 kwa Watoto chini ya miaka 14 na kilomita 5.0 kwa walio na miaka 15 na kuendelea. Pia itahusisha halaiki ya mazoezi (aerobics), breakdance” na mpira wa mezani (Teqball).

Siku ya Olimpiki husherehekewa kila mwaka tarehe 23 Juni, ikiwa kumbukumbu ya kuanzishwa kwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa hapo tarehe 23 Juni, 1894, Paris nchini Ufaransa.