Makamu wa rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Henry Tandau (katikati) tarehe 02/08/2023 amekabidhi Bendera ya Taifa kwa nahodha wa timu ya Tanzania ya Michezo ya Jumuiya ya Madola ya Vijana John Nahhay Wele katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za TOC. Kulia Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania Filbert Bayi.

Mashindano ya Jumuiya ya Madola ya Vijana yataanza tarehe 04/08/2023 nakumalizika 11/08/2023 huko Trinidad and Tobago, Port of Spain.